Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameonyesha kusikitishwa kwa kutotumika kwa gari ya wagonjwa uliofanywa na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambao wameshindwa kutumia gari hiyo kwaajiri ya kubeba wagonjwa jambo ambalo anasema kuwa kama Rais Magufuli akijua wataonekana ni watu wa ajabu.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Jijini Mwanza na kukuta dawa nyingi zilizopitwa na muda wake zikiwa zimehifadhiwa huku akiwa na wasiwasi na dawa hizo.

Amesema kuwa kurudishwa mtaani kwa dawa hizo na kuuziwa watu bila kujua kunaweza kusababisha matatizo makubwa, hivyo Mongella amesema ni lazima kuwe na utaratibu unaoeleweka kwa matumizi ya dawa hizo zilizopitwa na wakati ili kudhibiti zisiweze kurudi mtaani.

Aidha, ameongeza kuwa ameikuta gari hiyo ya kubeba wagonjwa ya Kagunguli ikiwa katika hospitali hiyo ya Nansio ambapo imesemakana kuwa imekuwepo hapo kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutumika huku watu wa Kagunguli wakikosa huduma ya gari la wagonjwa.

“Mkurugenzi naomba mtafuteni huyo dereva sasa hivi nikiwa hapa, tokea mwaka jana dereva wa Ambulance ya Kagunguli hayupo lakini nyinyi mnaniambia yupo mleteni hapa sasa nimuone, huyo dereva aje sasa hivi aondoke na diwani wa Kagunguli, diwani hata ukimuweka nyumbani kwako huyu dereva ni sawa tu, sasa dereva wa Kagunguli hospitali ya Nansio anafanya nini,”amesema Mongella

 

Msigwa: Tuko tayari kuuza kila kitu chetu kugharamia matibabu ya Lissu
Video: Mchungaji Mashimo amtabiria ushindi Uhuru Kenyatta