Serikali Mkoani mkoani Tabora  imeushauri uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Nyuki kuangalia uwezekano wa kuanzisha kozi za usimamizi wa mistu na uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na tatizo la uchomaji moto ovyo na uharibifu wa mistu ya asili.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati mahafali ya sita ya Chuo cha Mafunzo ya Nyuki kilichopo Tabora mjini, ambapo amesema kuwa hatua hiyo itasaidia wataalamu watakaokuwa wakisimamia na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuachana na tabia iliyojengeka miongoni mwao ya kupenda kuchoma moto ovyo.

Amesema kuwa hatua hiyo pia itakisaidia Chuo hicho kuongeza idadi ya wanachuo wanaodahiliwa hapo na hivyo kuongeza mapato yake ambayo yatawasaidia kutatua matatizo yakikabili Chuo na wanafunzi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wote ambao hawajawapelekwa kupata mafunzo zaidi ya ufugaji nyuki wawapelekwe haraka ili waweze kuwasaidia wafugaji wa nyuki  kuondokana ule ufugaji wa kizamani.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Nyuki, Semu Daudi amesema kuwa hivi sasa wameongeza udahili kwa ajili ya wataalamu wa nyuki kutoka wanachuo 34 mwaka 2010 hadi kufikia 205 mwaka huu.

Amesema kuwa lengo ni kutaka kuwepo na wataalamu wa kutosha ambao watasaidia kukuza sekta ya nyuki kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa viwanda hapa nchini na kuinua kipato cha wananchi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wanafundisha mbinu bora za ufugaji wa nyuki na ujasiriamali kwa lengo la kuwataka wataalamu hao waweze kwenda vijijini kuwasaidia wafugaji wa nyuki kuondokana na mbinu ambazo hazina tija kubwa kwao.

 

Mwanri azicharukia halmashauri Tabora
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 29, 2017