Michuano ya klabu bingwa iliendelea usiku wa jana ambapo michezo 8 ilipigwa katika viwanja tofauti, katika jiji la Manchestester wenyeji Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Shakhtar Donetsk mabao ya City yakifungwa na Kevin De Bruyne na Raheem Sterling.
Katika mchezo mwingine uliopigwa hapo jana usiku Real Madrid wakiwa ugenini kukabiliana na Borussia Dortimund waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku Cristiano Ronaldo akipachika mabao 2 na kujiwekea historia ya kipekee kwani mabao 23 kati ya 109 ambayo ni sawa na wastani wa 23% ambayo Cristiano Ronaldo amefunga katika Champions League amezifunga timu za Uherumani.
-
Video: Harry Kane apiga hat-trick ya kwanza klabu bingwa Ulaya
-
Man Utd wajiandaa kwa Paulo Dybala
-
Mipango ya timu za taifa za vijana
Liverpool walibanwa mbavu na Spartak Moscow baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 wakati Sevilla wakitwaa uongozi wa kundi E baada ya kupata alama 3 muhimu pale walipoifunga Maribor bao 3-0.
Harry Kane naye amezidi kudhihirisha ubora wake alionao baada ya kupiga hat trick wakati Tottenham wakiifunga Apoel bao 3 kwa 0 na kuwa mchezaji mwenye hat trick nyingi zaidi Ulaya katika msimu huu amefunga hat trick 7.