Mlinda mlango wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Manuel Neuer huenda asicheze tena msimu huu, kufuatia jeraha la mguu alilolipata wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Neuer aliumia mguu wa kushoto wakati wa muda wa nyogeza, baada ya miamba hiyo ya soka barani Ulaya kumaliza daklika 90 ikiwa imetoshana nguvu kwa matokeo ya jumla, kufuatia FC Bayern Munich kupata mabao mawili kwa moja.

“Manuel Neuer ameumia mguu, na tunahisi jeraha lake huenda likawa kubwa zaidi, lakini tunatarajia kupata majibu kamili atakapofanyiwa vipimo kesho (leo),” imeeleza taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani (fcbayern.com).

“Neuer atafanyiwa vipimo mjini Munich mara baada ya timu kuwasili ikitokea mjini Madrid nchini Hispania,” ilisomeka sehemu nyingine ya taarifa hiyo.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Real Madrid walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja, hivyo dakika 90 za mchezo wa jana zilipokamilika timu hizo zilikua zimefungana jumla ya mabao matatu kwa matatu.

Dakika 30 za nyongeza Real Madrid walifanikiwa kupata mabao matatu yaliyofungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao mawili dakika ya 105 na 110 kisha Marco Asensio dakika ya 112.

Kabla ya hapo FC Bayern Munich walikua wa kwanza kulisabahi lango la Real Madrid kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka nchini Poland Robert Lewandowski dakika ya 53 kabla ya Sergio Ramos hajajifunga dakika ya 84.

Dakika ya 76 Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la kusawazisha.

Mpina asema kero za Muungano zimepungua
LIVE: Maswali na Majibu Bungeni Dodoma