Bibi. Angela Vorobeva, raia wa Urusi amevunja rekodi ya dunia na kuingia kwenye kitabu cha orodha ya maajabu ya dunia cha Guinness baada ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi katika kilele cha Uhuru.

Bibi huyo alikuwa na umri wa miaka 86 na siku 267 alipoupanda Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa mita 5,895 na futi 19,340, mwezi Oktoba mwaka jana.

Kwa mujibu wa Guiness, Bibi. Vorobeva alitumia siku saba tu kufika katika kilele cha Uhuru. Aliondoka katika geti la Londorossi Oktoba 23 na kufika kileleni Oktoba 29. Oktoba 30 yeye na kundi la waongoza njia walianza kushuka mlima huo.

 

 

Venus Williams Atupwa Nje Australian Open
Wahariri wa Mawio wahojiwa na Polisi kwa Saa Nne, Jukwaa la Wahariri lapanga kumkataa Nape