Siku chache baada ya kujiunga na Lebo ya ‘WCB’, Rich Mavoko ameeleza jinsi ambavyo mpango wa kujiunga na lebo hiyo ulivyozaliwa na kukamilika akisisitiza kuwa hakumuomba Boss wake (Diamond) wala hakuombwa na Boss huyo.

Mavoko amefunguka Jumamosi iliyopita katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm alipiokuwa akizungumzia uanachama wake mpya kwenye lebo hiyo inayotabiriwa makubwa na kuleta mageuzi ya kimuziki nchini.

Alisema kuwa wazo la kujiunga WCB lilianza baada ya yeye kukutana na Meneja wa Diamond nchini Uganda katika tamasha moja ambapo Ambwene ‘AY’ Yesaya ndiye aliyeanzisha wazo la Mavoko kufanya kazi na meneja huyo.

Mavokofafanua kuwa baada ya mazungumzo, Salam alimwambia kuwa wanaweza kufanya kazi kwa njia fulani akiwa na Diamond pia, na ndipo alipoliwasilisha wazo hilo kwa Diamond kabla ya kulirudisha kwake.

“Salam aliniuliza, wewe una tatizo lolote na Nasibu (Diamond), nikamwambia sina tofauti yoyote na Nasibu. Alipomuuliza yeye pia akasema ‘sina tatizo na Rich’,” alieleza.

“Mimi sikumfuata Diamond wala Diamond hakunifuata mimi,” alisema.

Anasema Salam alikaa na uongozi wa Diamond pamoja na Diamond mwenyewe ambao waliliunganisha wazo hilo na mpango wao wa kufungua lebo, na yeye akawa sehemu ya waliokuwa kwenye mkakati wa kusainiwa.

Mavoko pia alikanusha taarifa zilizodai kuwa kuchelewa kwa mpango huo kulitokana na yeye kukataa ofa alizokuwa akiwekewa mezani na Diamond.

Msanii huyo hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wake wenye video kali ‘Itabaki Story’.

TFF Yapangua Kamati, Wakili Komba Apewa Kamati Ya Rufani Ya Nidhamu
Picha: Meninah afunga ndoa tena, ambwanga mtoto wa Muhongo