Mabingwa wa Soka nchini Nigeria Rivers United watawakosa wachezaji wao wawili tegemeo katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Young Africans.

Mchezo huo utakaoamua nani anakwenda Nusu Fainali ya Michuano hiyo, utapigwa jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Young Africans ikiwa na faida ya mabao mawili waliyoyapata kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa nchini Nigeria mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili Aprili 23).

Kwa mujibu wa Mtandao wa Rivers United, timu hiyo itamkosa beki wa kushoto, Ebube Duru na kiungo mshambuliaji, Williams Ukeme.

Mtandao huo umeeleza kuwa, kuna uwezekano wa timu hiyo ikamkosa mshambuliaji wao tegemeo, Paul Acquah ambaye alikosekana katika mchezo uliopita kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Mshambuliaji huyo bado hajaanza mazoezi na wenzake, hadi wakati wakiwa katika maandalizi ya safari ya Dar es salaam-Tanzania kucheza dhidi ya Young Africans.

“Wakati timu ikijiandaa na safari ya kuelekea Tanzania kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili dhidi ya Young Africans, huenda tukawakosa wachezaji wetu muhimu wawili hadi watatu.”

“Wachezaji wote hao wana majeraha, Ebube na Ukeme walipata majeraha katika mchezo dhidi ya Young Africans, mwishoni mwa juma lililopita.”

“Acquah alipata majeraha katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, hivyo ni pigo kwetu kuelekea mchezo huo wa Mkondo wa Pili dhidi ya Young Africans,” imeeleza taarifa hiyo

Katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza Uliopigwa Uwanja wa Godswill uliopo katika Mji wa Uyo, Nigeria, Young Africans ilipata mabao yake mawili kutoka kwa Mshambuliaji wao Fiston Mayele, rais wa DR Congo.

Young Africans inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote dhidi ya Rivers United ili kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku wageni wao wakihitaji ushindi wa mabao 3-0 ama zaidi ili kujihakikishai nafasi ya kusonga mbele.

Museveni ataka sababu kwanini mwanae asiwe Rais
Cheza Sloti ya Blackjack Live Ushinde Mara 100 ya Dau Lako