Mshambuliaji kutoka nchini Poland, Robert Lewandowski, usiku wa kuamkia hii leo alifanikiwa kuisaidia FC Bayern Munich kupata ushindi mnono wa mabao matano kwa moja dhidi ya VFL Wolfsburg katika mchezo wa ligi ya nchini Ujerumani.

Lewandowski, aliwashangaza walio wengi katika mchezo huo kutokana na kufanikiwa kufunga mabao matano kwa mguu wake na kuweka rekodi ya kipekee tangu msimu huu ulipoanza nchini Ujerumani.

Lewandowski, alifunga mabao hayo katika dakika ya 9 za mchezo huo ambao uliunguruma kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Mabao hayo ya kustaajabisha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika dakika ya 51, 52, 55, 57 na 60.

Hata hivyo wageni Wolfsburg walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika mchezo huo ambalo lilifungwa na Daniel Caligiuri, katika dakika ya 26.

Meneja wa FC Bayern Munich Pep Guardiola, alimwagia sifa kedekede Robert Lewandowski, kwa kusema ameonyesha ujasiri na uhodari wa kipaji alichojaaliwa na imekua ni faida kwa kila mmoja kikosini mwake kujivunia mchezaji wa aina hiyo.

Amesema ilikua ni vigumu kuamini kama Robert Lewandowski, amefanikisha ushindi wa mabao matano walioupata ndani ya dakika 9, lakini ilimlazimu kuamini kutokana na mazuri ambayo amekua akiyaona mazoezini kutoka kwa mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na FC Bayern Munich mwaka 2014 akitokea Borussia Dortmund.

Robert Lewandowski, aliwahi kufunga mabao mnne pekee yake katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, wakati akitumikia Borussia Dortmund na mazuri hayo aliyafanya katika matanange wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Real Madrid mnamo April 24 mwaka 2013.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya nchini Ujerumani iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Darmstadt 2 – 1 Werder Bremen

Hertha Berlin 2 – 0 FC Cologne

Ingolstadt 0 – 1 Hamburger SV

Ni Mzunguuko Watatu Capital One Cup
Arsene Wenger Aachana Na Mkewe