Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino, ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kitaingia kambini mwishoni mwa juma lijalo kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga amelazimika kufanya maamuzi ya kumuondoa mshambuliaji huyo, baada ya kupata majeraha akiwa katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi nchini England *Capital One cup* ambapo Liverpool waliwashinda Carlisle United kwa njia ya mikwaju ya penati mitatu kwa miwili.

Firmino, alilazimika kufanyiwa mabadiliko wakati wa mchezo wa kombe la ligi na baadae alibainika amepata majeraha katika sehemu za goti la mguu wake wa kulia.

Nafasi ya Firmino imechukuliwa na mshambuliaji wa klabu ya AC Milan ya nchini Italia Ricardo Oliveira.

Kocha Dunga amesema Ricardo mwenye umri wa miaka 35, anatosha kuziba nafasi ya Firmino kuelekea katika michezo miwili ya kusaka naafsi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyikwa nchini Urusi dhidi ya Chile na kisha Venezuela.

Oliveira, ameshabahatika kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil mara sita tangu mwaka 2006.

Timu ya taifa ya Brazil, haijawahi kushindwa kufuzu katika fainali za kombe la dunia.

Pato: Nilikataa Kurudi Ulaya
Busungu Aomba Angalau Dakika 30