Kataaika hali isiyotarajiwa, Rais William Ruto alimnyamazisha mkalimani wa Ikulu ya Tanzania wakati wa hotuba kwa wanahabari aliyofanya kwa pamoja na Rais wa Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Jumatatu, Oktoba 10, Rais Ruto alimnyamazisha mkalimani huyo ambaye alianza kutafsiri hotuba yake kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili bila kumtaarifu Rais Ruto.

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia

Rais huyo wa Kenya alilazimika kusitisha hotuba yake na kuuliza kipi alichotaka afisa huyo wa kikosi cha mawasiliano cha Rais Samia na baadaye Mkalimani huyo alifafanua kuwa hatua yake ilikuwa kuwezesha vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa umma.

“Sidhani kama kuna haja ya kutafsiri. Kuna mtu haelewi Kiingereza hapa? Wananchi? Haya nitarudia, nitarudia baadaye. Wewe utanichanganya zaidi. Pole,” Ruto alisema.

Awali, Ruto alikiri kuwa alikuwa ametatizika kuzungumza Kiswahili ambayo ndio lugha rasmi ya Tanzania.

“Mtukufu Rais, nimetatizika na Kiswahili asubuhi hii kwa sababu kimenichanganya sana. Naomba uniruhusu nihutubu kwa lugha ya Kiingereza ili nieleweke vyema,” Ruto alisema.

Hata hivyo Ruto aliahidi kuwa kwa ziara za mara kwa mara nchini Tanzania, ataimarisha Kiswahili chake ili kutotatizika na kuhitaji mkalimani.

Ujenzi Bomba la gesi kupunguza gharama za Nishati
Kim afurahia kukamilisha shamba la mboga