Vyombo vya Habari vya Korea Kaskazini, vinasema kiongozi Kim Jong Un alihudhuria sherehe siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa shamba moja kubwa la mboga nchini humo.

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo ilionyesha picha za Kim akizuru majengo ya kuhifadhi mazingira katika mkoa wa mashariki wa Hamgyong Kusini, na kutoa maagizo kwa maafisa wakuu.

Shamba hilo, lililojengwa kwenye tovuti ya kituo cha anga kilichobomolewa, likisemekana kuwa mradi muhimu wa Kim ambaye alikuwa ameamuru likamilike kufikia Oktoba 10, 2022 wakati Chama tawala cha Wafanyakazi nchini humo kilipoadhimisha miaka 77 tangu kuanzishwa kwake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un akitazama zao la nyanya kwenye moja ya mashamba ambayo ya mbogambona nchini humo. Picha na Reuters.

Zaidi ya greenhouses 800 zimejengwa kwenye makazi ambapo Gazeti la chama hicho, Rodong Sinmun, linasema kuwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa chama hicho kwenda kwa wananchi.

Kim, anasemekana kuwaagiza maafisa kujenga mashamba makubwa ya aina hiyo katika maeneo mbalimbali ili kusambaza mboga nyingi kwa wananchi.

Gazeti hilo, liliripoti siku ya Jumatatu kwamba Kim alisimamia mazoezi ya kijeshi ya vitengo vya mbinu za kinyuklia a ziara yake katika kituo hicho cha kilimo wakati wa maadhimisho ya kuanzishwa kwa chama tawala inaaminika kuwa inalenga kuwaonyesha watu wa Korea Kaskazini kwamba anafanya kazi pia kuboresha maisha yao.

Ruto amnyamazisha mkalimani wa Samia
Sindano zatumika kuua watoto hospitali