Mawaziri Wakuu wa Algeria na Ufaransa wameelezea nia yao ya “kuimarisha” uhusiano wa joto baada ya kuongezeka kwa maelewano kati ya marais wa nchi hizo mbili mwishoni mwa mwezi Agosti 2022.

Matakwa na nia hiyo, imeelezwa jijini Algiers, hapo jana Oktoba 9, 2022 ikiwa mwanzoni mwa ziara ya siku mbili ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, Elizabeth Borne pamoja na wajumbe 15 wa ngazi ya juu alioongozana nao.

Kulingana na Azimio la Algiers, katika kipindi cha miezi michache iliyopita majadiliano yao yamelenga kusimamia na kupanga vyema mienendo ya watu kati ya nchi hizo mbili huku wakijadili njia za kuhimiza uhamaji wa wanafunzi, kisayansi na kisanii na kiuchumi.

Aidha, Borne amezitaja nguzo tatu za ushirikiano huo “ulioimarishwa wa kukuza biashara, uvumbuzi na kutengeneza ajira ikiwemo uhamaji na visa sambamba na vijana wanaotakiwa kuongeze ushirikiano wa kielimu na kitamaduni.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Algeria, Aïmene Benabderrahmane, amesema “Tumebainisha pamoja ubora wa mazungumzo ya kisiasa kati ya nchi zetu kwa ngazi zote na hasa kati ya marais wa nchi hizi na makubaliano madhubuti juu ya suala muhimu la kuimarisha mashauriano na uratibu kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja.”

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Elisabeth Borne alianza ziara yake katika nchi hiyo kwa ishara za ukumbusho, akifuata mfano wa Rais wake, Emmanuel Macron wakati wa safari yake mwishoni mwa Agosti 2022, ambayo baada ya miezi ya mvutano, ilisaidia kurudisha uhusiano wa joto kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Rais wa Kenya nchini yajibu maswali ya Wananchi
Kikosi kazi chavuruga ngome ya Al-Shabaab kibabe