Rais wa Kenya, William Ruto, ametoa wito kwa Majenerali wanaopigana nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake Mohamed Hamdan Daglo kusitiha vita
Ruto ametoa wito huo huku akisema kupigana ni kitendo ambacho cha kipumbavu na kutaka Umoja wa Afrika kutafuta njia muafaka ya kutatua migogoro barani Afrika.
Akizungumza na Wabunge wa Bunge la Afrika nchini Afrika Kusini amesema wakati huu ambapo mapigano kati ya pande mbili za kijeshi nchini Sudan yakiingia mwezi wa pili sasa ni lazima suluhu ipatikane ili kunusuru watu wasio na hatia.
Mapigano mazito yamekuwa yakiendelea jijini Khartoum, na miji mingijne ya Bahri na Omdurman licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kusitishwa kwa vita ambayo yamekuwa hayaheshimiwi na pande zote mbili.