Vita vinavyoendelea nchini Sudan, vimewakutanisha wasomi wa jadi waishio mijini ambao kwa muda mrefu wameshikilia mali na mamlaka katika mji mkuu wa Khartoum dhidi ya vikosi vingine vya vijiji vilivyotengwa kujadili hatma yao.

Hatua hiyo, inatokana na muda wa zaidi ya mwezi uliopita majenerali wawili mahasimu wanapigania udhibiti wa kimamlaka katika Taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika yaliyosababisha kueneza vurugu, na kusababisha vifo vya karibu watu elfu moja na kuwakosesha makazi karibu milioni moja.

Majenerali hao ni Mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al Burhan ambaye ni mwanajeshi wa siku nyingi na mzaliwa wa kaskazini mwa khartoum awali alimpindua kiongozi wa kiislamu wa muda mrefu Omar al-Bashir, baada ya maandamanano makubwa na kisha kuchukua madaraka kamili mwaka 2021.

Mwingine ni Makamu wake wa zamani, Mohamed Hamdan Daglo ambaye aliwahi kuwa mfugaji ngamia kutoka mkoa wa magharibi wa Darfur, unaopakana na Chad ambaye sasa anaongoza kundi la wanamgambo wa Jeshi la akiba – RSF.

Kocha Simba SC aficha usajili 2023/24
Young Africans yajinadi kuimarika 2023/24