Zaidi ya watu 27 wamepoteza maisha nchini Rwanda, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo, Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo huku idadi ya walifariki ikitarajia kuongezeka.
Taarifa za vyombo vya Habari nchini humo zinasema maeneo ya Magharibi hasa ya Wilaya za Rutsiro, ndiyo yaliyoathiriwa zaidi, wakati huu kukiwa na wasiwasi kuwa huenda madhara zaidi yatokanayo na maafa hayo yakaongezeka.
Zaidi ya watu 120 wamethibitishwa kufariki katika maporomoko ya udongo Rwanda. Picha ya REUTERS.
Afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Rwanda, Emmanuel Mazimpaka ni amesema, “kumenyesha mvua kubwa, kuna mito ambao kingo zilivunjika na kukawa na maporomoko ya udongo ambayo yalisababisha maafa makubwa.”
Serikali ya Rwanda inasema kuwa juhudi za kuwatafuta watu waliopotea zinaendelea na pia inafanya juhudi kuwaokoa watu walio hai baada ya kutokea mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo, Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu 127 wamepoteza maisha.