Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefanya msako maalum katika maduka yanayouza sukari mjini Boma’ngombe na kukamata Wafanyabiashara 7 waliokiuka maagizo ya serikali kwa kupandisha Bei kutoka sh 2,700 hadi 3,500.
Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kukamatwa kwa watu hao na kufungwa kwa maduka yao kwa kukiuka maelekezo ya serikali na kutumia Ugonjwa wa Corona na mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwanyanyasa wananchi.
”waliopandisha bei ya sukari kwenye wilaya hii kutoka bei ya sh 2,700 maelekezo ya serikali mpaka 3,000 wafungiwe maduka mpka watakapotuletea barua za kutuambia ni kwanii tusiwafugie lakini maduka yasifunguliwe na dola itachua hatua zake za kinidhamu kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifuu”. Amesema DC Sabaya.
Ukaguzi huo umefanyika baada ya Mkuu wa wilaya kutuma watu kwa siku tatu mfululizo kujua mienendo ya biashara hiyo wilayani hapo.