Senegal wamefuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Afrika Kusini katika uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane jana.

Sadio Mane alichangia sana ushindi huo wa Simba wa Teranga na wanarejea baada ya miaka 16 kushangaza watu wakicheza katika Kombe la Dunia mara ya kwanza, michuano iliyoandaliwa Korea Kusini na Japan mwaka 2002.

Mane alitoa pasi safi kwa mshambuliaji wa West Ham Diafra Sakho aliyefunga bao dakika ya 12 kabla ya winga huyo wa Liverpool kufunga bao la pili zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya muda wa mapumziko.

Winga huyo wa Liverpool kisha alisaidia kushinda mechi hiyo kwa kuchangia bao la pili dakika mbili kabla ya muda wa mapumziko.

 

Timu zote mbili zitakutana tena Dakar Jumanne katika mechi ambayo itakuwa ya kutimiza wajibu tu kwani Senegal wamejiunga na Nigeria na Misri katika orodha ya nchi ambazo zimefuzu Kombe la Dunia.

Diamond afunguka ujio wa ngoma yake na Rick Ross
Patrice Evra afukuzwa Marseille