Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Tuchel amekutana na Mshambuliaji Harry Kane lakini ishu ya kumnasa mshambuliaji au la itategemea na hatima ya mkali Sadio Mane.

Mshambuliaji huyo zamani wa Liverpool, Mane amekuwa akiripotiwa kwamba anaweza kuachana na Bayern kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, huku ikielezwa huenda akarudi kwenye Ligi Kuu England.

Mambo yameshindwa kwenda sawa kwa Msenegali huyo tangu alipojiunga na mabingwa hao wa Bundesliga kwa ada ya Pauni 35.1 milioni mwaka jana.

Jambo hilo limemfanya Mane hata kuhusishwa na Manchester United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi wakati wakitafuta kujiimarisha kwenye fowadi.

Huko nyuma Mane alishawahi kuhusishwa na Man United kabla ya kuamua kwenda Liverpool. Kwingine anakohusishwa Msenegali huyo ni Saudi Arabia.

Hata hivyo, kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, Mane hakufuta uwezekano wake wa kuendelea kubaki kwenye kikosi cha FC Bayern Munich msimu ujao.

Mane alipoulizwa kama atabaki Bayern alisema: “Ndio, Mungu akipenda. Kama mambo yatakwenda vizuri, nitarudi Bayern. Napenda changamoto na Bayern ni changamoto kubwa. Ni jukumu langu la kupambana kwa kila namna kukabiliana na changamoto hizo. Ni kawaida.”

Hiyo ina maana kama Mane atabaki Bayern, basi mabosi hao wa Allianz Arena hawatakuwa na jeuri ya kutumia pesa nyingi kwenye kumnasa straika wa Tottenham Hotspur, Kane kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, wakati wakiwa bize kujaribu kutafuta fowadi wa kuja kuziba pengo la Robert Lewandowski, aliyetimkia Barcelona mwaka jana.

Juma Said Nyosso kurudi Kagera Sugar
Djuma, Bangala wanasepa Young Africans