Baada ya kuripotiwa kumalizika kwa mvurugano wa kugombea kupiga penati baina ya Edinson Cavani na Neymar uliotokea wiki chache zilizopita mapya yameibuka juu ya sakata hilo.
Iliripotiwa kuwa Neymar aliomba radhi kwa klabu ya PSG lakini inasemekana baadae mabosi wa klabu hiyo walikaa chini na Edinson Cavani na kumuomba amruhusu Neymar kupiga penati huku pia wakitaka kumpa kiasi cha pesa ili akubali.
PSG walitaka kumpa Cavani kiasi cha Euro milioni moja (€1million) ambacho ni kiasi cha pesa ambayo wangempa mwisho wa msimu kama akimaliza akiwa mfungaji bora lakini sasa wakataka kumpa kiasi hicho ili amuachie Neymar kupiga matuta.
-
Neymar hamtaki kabisa Cavani, aomba PSG imuuze
-
Edinson Cavani avunja rekodi ya Ibrahimovic
-
Fran Escriba afukuzwa Estadio de la Cerámica
Edinson Cavani amekataa kiasi hicho cha pesa na hii inamaanisha kwamba hayuko tayari kumuachia mtu mwingine apige penati na anaona ni bora akose kiasi hicho cha pesa kuliko kuacha kupiga penati.
Kibaya zaidi ni kwamba kumeanza kuwa na makundi katika klabu hiyo hali inayomuweka njia panda kocha wa klabu hiyo Unai Emery kwani ni wazi na yeye anataka Cavani aendelee kupiga penati katika timu hiyo lakini tajiri wa timu hiyo Nasser El Khaifi anaonekana anataka Neymar awe kila kitu.
Katika klabu hiyo sasa inasemekana kuna kundi kubwa linalomuungamkono Cavani huku kikundi kingine kidogo kinachoundwa na wabrazili peke yao wakiwa upande wa Neymar.