Viongozi wa Mataifa mbalimbali duniani kote wameendelea kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Kongozi wa zamani wa kanisa katoliki, Papa Benedict wa 16, aliyefariki akiwa na umri miaka 95.
Wengi wa Viongozi hao, wamesema Dunia imempoteza mwanathiolojia aliyekuwa na ushawishi mkubwa na kwamba alikuwa ni nguzo ya imani na busara ambapo dunia itaendelea kumkumbuka.
Waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Waziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kwa nyakati tofauti wamemsimulia Papa Benedict kuwa ni alifanya kazi kwa moyo na busara.
Aidha, Mazishiya Papa Benedict wa 16 yanatarajia kuongozwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kwenye kanisa kuu la mtakatifu Petro Januari 5, 2023.