Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Samia Suluhu Hassan amehitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022, ambazo zimefikia kilele chake Wilayani Bukoba Mkoani Kagera.
Samia amehitimisha mbio hizo baada ya kupokea mwenge huo wa uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio hizo Kitaifa, Sahil Geraruma kwenye uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba, Mkoani Kagera hii leo Oktoba 14, 2022.
Viongozi mbalimbali walipokuwa wakisubiri kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan wakiongozwa na Mkuu wa Mkao wa Kagera Albert Chalamila. (wa kwanza kushoto)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio hizo Kitaifa Sahil Geraruma katika Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022.
Vijana wa Halaiki wakionesha kazi mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera hii leo Oktoba 14, 2022.
Vijana wa Halaiki wakitumbuiza kwa kuonesha kazi mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera, Oktoba 14, 2022.