Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango wamehudhuria misa takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki, Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera

Rais Samia, ambaye pia ni amiri Jeshi Mkuu amehudhuria misa hiyo hii leo Oktoba 14, 2022 siku ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, akiongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, Mapadri pamoja na viongozi mbalimbali.

Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini, Mapadri pamoja na viongozi mbalimbali, mara baada ya Misa Takatifu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki, Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera hii leo Oktoba 14, 2022.

Hofu ya misaada chanzo ukimya wa Afrika sakata la Ukraine
Taifa lisilo na utamaduni wake ni Taifa mfu: Julius K. Nyerere