Watu 18 wa familia moja wakiwemo watoto 12, wamefariki baada ya basi waliyokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya mfumo wa umeme.

Afisa wa Polisi wa eneo la Javed Baloch nchini Pakistan, amesema baadhi ya miili imeharibiwa na moto kiasi cha kutotambulika.

Basi hilo, lilikuwa limewabeba watu 50 wenye uhusiano wa kindugu wakitokea mji wa kusini wa Karachi kuelekea Jimbo la Sindh.

Familia hiyo ilihamia Karachi mwezi Agosti baada ya mji wao wa “Khairpur Nathan Shah” kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 nchini humo.

Barabara mbovu, magari yasiyotunzwa vizuri na mfumo duni wa usalama barabarani husababisha kila mwaka ajali nyingi nchini Pakistan na kulingana na takwimu za serikali, ajali hizo husababisha maelfu ya vifo.

Kisa Ebola: Museveni apiga marufuku 'Sangoma'
Taarifa: Kopafasta Microfinance Limited haina uhusiano na ile iliyotajwa BRELA