Mwanajeshi mmoja wa Nigeria amekamatwa na Kikosi cha Jeshi lake kwa tuhuma za kuiba na kuuza risasi kwa magenge ya wahalifu na makundi ya kigaidi.

Mshukiwa huyo, aliyetambulika kwa jina la Lorliam Emmanuel, anasemekana kufanya kazi chini ya kikosi cha askari 156 huko Mainok, kilichopo jimbo la Borno.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewana na Zagazola Makama wa eneo la LakeChad, mwanajeshi huyo alinaswa akiwa na risasi alipokuwa akitoka mji mkuu wa jimbo hilo, Maiduguri.

Mshukiwa, Lorliam Emmanuel, mwanajeshi wa kikosi cha askari 156 huko Mainok, Nigeria. Picha na NDN.

Katika video iliyosambazwa na chapisho hilo, wanajeshi walionekana wakimvua mshukiwa risasi zilizokuwa zimefungwa kwenye mwili wake ambazo tayari alikuwa amehifadhi kwa ajili ya kuziuza kwa waasi.

Wanajeshi wenzake walisikika wakisema, “Unaona maisha yako? Wewe, utaenda kuwapa Boko Haram vitu hivi ili waje kutushambulia katika kambi hii usijali Mungu akulinde.”

Zagazola Makama anasema, mshukiwa huyo anayetoka Benue, mara kwa mara huiba risasi na vifaa na kuviuza kwa kwa magenge ya wahalifu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 13, 2022    
Baraza la Wafanyakazi lajadili usalama sehemu za kazi