Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA), Mkoani Kagera kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya jamhuri ya China kwa gharama ya zaidi ya Shilingi 22 Bilioni kikiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya Wanafunzi 1,400.

Uzinduzi wa chuo hicho, umefanywa na Rais Samia hii leo Oktoba 13, 2022 Mkoani Kagera na kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi hao kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu wa fani mbalimbali za ufundi na huduma kikiwa na karakana, vifaa na miundombinu ya kisasa.

Chuo hicho ambacho kina ofisi za Walimu wanane, nyumba tatu za walimu, bweni lenye uwezo wa kuhudumia vijana wa kike 214, na wakiume 116, kina uwezo wa kuchukua vijana 400 wa kozi za muda mrefu na 1,000 wa kozi za muda mfupi na kikiwa na madarasa yatakayohudumia watu 218 kwa pamoja na maktaba yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 30.

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda katika ukaguzi wa maandilizi ya halfa hiyo alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kujiunga na mafunzo mbalimbali yanatolewa katika chuo hicho.

Taarifa: Kopafasta Microfinance Limited haina uhusiano na ile iliyotajwa BRELA
Wakurugenzi wapya TAWA kutekeleza mikakati kuzuia ujangili