Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta jijini Nairobi.

Aidha, Makamu wa Rais ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba ambapo wamepokelewa na balozi, Robinson Njeu Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini humo, Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta zitafanyika katika uwanja wa Kasarani uliopo jijini Nairobi ambapo ataiongoza Kenya kwa muhula wa pili.

LIVE KENYA: Kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta
Usalama waimarishwa sherehe za kuapishwa Kenyatta