Kampuni ya Samsung Electronics Ltd. Imezindua matoleo mapya ya simu za Galaxy S23+ na Galaxy S23 ikikaribisha zama mpya za matumizi ya simu yenye hadhi ya premium, ambapo Kamera zake zitawapa watumiaji uhuru wa kuonesha ubunifu kama vile kupiga picha zenye hadhi ya kisinema nyakati za usiku na video zenye uwezo wa Artificial Intelligence yenye teknolojia ya kujiongoza ya kisasa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi wa simu aina ya Samsung Galaxy S23 Ultra, Galaxy S 23+ na Galaxy S 23, Mkuu wa Kampuni hiyo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, Manish Jangra alibainisha kuwa Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimekuwa na mchango mkubwa wa katika kukuza bidhaa za simu zao.
Simu hizo, pia zinatoa uwezo wa kucheza gemu nyingi na nzuri kwani ina graphics zenye hadhi ya juu na zilizo na spidi na huja na S Pen yake ambayo watumiaji wengi wanafahamu na kupenda matumizi yake na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa kalamu hiyo na simu zote za Samsung zina uwezo mpya wa hali ya juu kiteknolojia na muonekano maridhawa ambao unaendelea kuonesha kujali kwa matumizi mbadala ya vifaa, ili kutunza mazingira ambayo Samsung huzingatia.
Alisema”simu zetu kwa hakika ni bora na zimekuwa zinakubalika sehemu mbalimbali duniani na kinachoangaliwa kwa sasa ni namna ambavyo simu hizi zinachangia katika maendeleo ya shughuli za teknolojia na taifa kwa ujumla na Galaxy S23 Ultra 512 GB itauzwa kwa 3,830,000 TZS, Galaxy S23 Ultra 256 GB itauzwa kwa 3,510,000 TZS, Galaxy S23+ 256 GB itauzwa kwa 2,780,000 TZS na Galaxy S23 256 GB itauzwa kwa 2,440,000 TZS.”
Aidha, ameongeza kuwa, huduma zinazopatakana kwenye simu hizo ni bora na zimekuwa zikichangia katika nyanja mbalimbali za kukuza uchumi ambapo alitolea mfano wa kamera za kisasa katika simu ambazo zimekuwa zikitumiwa kwenye shughuli mbalimbali nje ya mawasiliano ya kawaida.
Jangra amesema, simu hizo zina uwezo mkubwa wa aina mbalimbali katika ufanyaji wake wa kazi hasa kwa kutoa picha bora hata kwenye mazingira ya giza, ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi data na ina gallery kubwa yanye uwezo wa kuhifadhi picha.
Kwa upande wake, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Samsung Afrika – BS Hong alibainisha kuwa kwa mwaka jana simu ya Samsung Galaxy S 22 ilifanya vema sokoni na kwa sasa kampuni hiyo ina imani kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki simu zake hizo mpya za Galaxy S23 zitauzwa kwa wingi hasa kutokana na ufanisi wake mkubwa.