Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza Mshambuliaji wa klabu ya Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah (Karihe) ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Afrika mashariki na kati (Challenge CUP), itakayoanza Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017 nchini Kenya.
Karihe ambaye aliifungia Lipuli FC bao la kwanza msimu huu wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara wakati wa mchezo dhidi ya Young Africans kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam, anaongeza idadi ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes na kufikia 31.
“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe kwa sasa ataungana na wenzake.” Alisema Morocco.
Kikosi cha awali kilichotajwa na kocha Morocco kina wachezjai kama Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi),Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU), Abdallah Haji “Ninja” (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh “Machupa” (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame “Luiz” (Mlandege), Issa Haidar “Mwalala” (JKU), Abdulla Kheir “Sebo” (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).
Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma “Zimbwe” (Chipukizi), Mohd Issa “Banka” (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman “Pwina” (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Academy Spain), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim “Seleembe” (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa “Rais” (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).