Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema atazifumua Sekretariet za Mikoa endapo hazitatekeleza majukumu yake ipasavyo.
Waziri Ummy ameyasema hayo alipokua akizungumza na Sekretariet ya Mkoa wa Tanga katika Ukumbi wa Ofiso ya Mkuu wa Mkoa Mkoani hapo.
Waziri Ummy amesema jicho lake la karibu ni Sekretarieti za Mikoa ambapo amesema kuwa hategemei kupambana na Halmashauri 184 wakatiSekretarieti za Mikoa zipo.
‘Sitaki kuona Sekretarieti za Mikoa ni watu wa ‘kucompile’ taarifa za Halmashauri tu ninataka kuona zinakaa na Halmashauri zao zinawashauri, mnaweka mambo sawa na mnazisimamia ipasavyo katika utekelezaji wa majuku yako ya kila siku’ amesema Waziri Ummy
Aidha amesema Sekretariti ya Mkoa ambayo atabaini kuwa wataalam wake ni wazembe na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo itabidi wapishe wawekwe watu watakaochapa kazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu huku wakienda na muda.
Waziri Ummy amezitaka Sekratariet za Mikoa kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri zilizoko kwenye Mikoa yao, Matumizi ya Fedha za mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupeleka fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo na utoaji wa mikopo ya asilimia kumi huku wakisimamia marejesho ya mikopo hiyo ili izunguke kwa wananchi wengine wafaidike na mikopo hiyo.