Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema Wizara hiyo inayo majukumu makubwa iliyopewa na Serikali ikiwemo kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.
Dkt. Biteko ameyasema hayo hii leo Machi 10, 2023 kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara na Tasisi zake kilichofanyika jijini Dodoma wakati akimkaribisha na kumtambulisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo.
Amesema, kazi iwe ni kipimo cha ukaribu cha utendaji wa kazi kwa watumishi wa wizara na taasisi katika kufikia malengo hayo na kuongeza kwamba, Wizara itaendelea kuweka mazingira bora ya kazi kwa watumishi pamoja na taasisi zilizopo chini yake ili kukuza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kheri Mahimbali akiwataka Wataalam Sekta ya Madini kuweka Msukumo katika Madini na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mbibo akiwakumbusha watumishi kutambua matarajio ya Watanzania kwenye Sekta ya Madini nchini.