Hatimaye siku iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu na Watanzania ya kuishuhudia timu yao ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefika ambapo, leo Jumatatu inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.
 
Aidha, Serengeti Boys imepangwa katika Kundi B, ambapo katika kundi hilo iko pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.
 
Hata hivyo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa kikosi cha Serengeti Boys kiko vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa mali kwenye mchezo huo wa kwanza.
 
“Kikosi kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,” amesema Bakari Shime.
 
Timu hiyo ya Taifa ya vijana pamoja na maandalizi mazuri lakini imepata pigo baada ya nahodha, Abbas Makamba kuvunjika mguu hivyo hataweza kushiriki mashindano yote.

Manara alalama kubambikiwa mzigo usiomhusu
?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 15, 2017