Hali ya Utoaji wa vyandaru nchini imekuwa katika hali nzuri licha ya kuwa matumizi yake bado hayaridhishi na Serikali inaendelea na kampeni ya kuhamaisha jamii juu ya matumizi sahihi ya hitaji hilo.
Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti na Kutokomeza Malaria, Dkt. Abdalah Losasi ameyasema hayo na kuongeza kuwa mikakati ya wizara ni kuhakikisha wanapunguza wingi wa ugonjwa wa malaria na kutoa tiba kinga ya malaria kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja.
Amesema, “elimu ikitolewa itafanikisha kubadilisha tabia ya mwananchi sasa akibadili tabia atatumia na kumbadilisha mtu ni hatua wengine wanasema matumizi yake ni vyandarua,Mpango wa muda mrefu ni kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.”
Aidha Dkt. Losasi ameongeza kuwa, “tunataka kutoa tibakinga kwa watoto walioko shule ya msingi imebainika kuwa katika mikoa yenye maambukizi ya juu wanaishi na vimelea vya malaria tafiti zinaonesha dawa zinaweza kusaidia kwa asilimia 80 kupunguza malaria.”