Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa Serikali imeandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa biashara ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji.

Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu maswali na hoja za mbalimbali za wabunge.

“Biashara ya Chuma chakavu imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla,na hili limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na wahalifu kuaharibu miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili waiuze kama chuma chakavu”Alisema Mwijage.

Aidha, amesema kuwa ili kukabiliana na hujuma hizi ni lazima Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS  na  RAHACO kufanya kazo kswa ushirikiano wa karibu na Jeshi la Polisi ili kuweza kukabiliana na wizi wa rasilimali zao.

Mwijage amesisitiza kuwa Muswada huo umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu hiyo.

Hata hivyo, Mwijage ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi wanapoona mtu anayehujumu  miundombinu kwa namna yote ile.

 

Samia Suluhu aagiza ushirikiano katika utunzaji mazingira
Serikali yaandaa utaratibu wa kukuza sekta ya Tumbaku nchini