Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, William Ole Nasha amesema kuwa Serikali  inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku  kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.

Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge.

“Serikali ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku,”amesema Ole Nasha.

Ole Nasha amesema kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.

Aidha, amezitaja pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa kuzingatia wakulima wanahitaji huduma muhimu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia masuala hayo.

 

Serikali kuwadhibiti wafanyabiashara wa chuma chakavu
FC Barcelona Waombwa Kumsajili Paulo Dybala