Serikali imeanza mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho kutoka tani 315,000 mpaka tani milioni moja ifikapo mwaka 2023 lengo ikiwa kukuza uchumi wa wakulima nchini.
Wizara ya Kilimo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI), kwa kushirikiana na Bodi ya korosho Tanzania pamoja na Halmashauri Kupitia mkakati huo, imeeendesha mafunzo kwa kutoa mbinu za kilimo bora cha zao la korosho hapa nchini.
Mratibu wa zao la korosho kutoka TARI Dkt. Geradina Mzena, amesema lengo la uzalishaji ni kuongeza ulimaji wa zao la korosho kutoka mikoa mitano inayolima korosho hivi sasa na kufikia mikoa 17.
Mafunzo hayo yamewahusisha maafisa ugani na wakulima katika halmashauri ya mlimba, ifakara, malinyi na ulanga.
Mikoa iliyopo katika mikakati ni Morogoro,Iringa,Dodoma,Singida,Tabora,Katavi,Kigoma,Songwe, Ruvuma Mbeya,Kilimanjaro na Njombe.