Serikali ya Libya imetangaza hali ya hatari mara baada ya kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli na maeneo yaliyo karibu na mji huo, ambapo watu zaidi ya 39 wamefariki na wengine kujeruhiwa.

Libya imetangaza hali hiyo ili kuweza kuwalinda raia wake, mali pamoja na asasi muhimu kwa jamii nzima na wageni wanaoingia nchini humo.

Aidha, Serikali hiyo ya Libya imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha uhasama.

Hata hivyo, wakati yakitokea hayo, takriban wafungwa 400 wametoroka kutoka gereza moja kusini mwa Tripoli, eneo ambalo pia limeshuhudia mapigano makali katika kipindi cha wiki moja kati ya makundi hasimu.

 

Yaya Toure atimiza ahadi, arudi Olympiakos
LIVE: Rais Magufuli katika hafla ya uwekaji saini mikataba ya ujenzi wa meli mpya