Serikali imekiagiza Chuo cha Diplomasia kujikita katika kuongeza tafiti pamoja na machapisho mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wahitimu wa chuo hicho kutoa mchango wao katika Taifa hususani wakati huu wa utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipotembelea chuo hicho na kuongea na wahadhiri, wafanyakazi pamoja na wanafunzi.
“Utafiti na machapisho siyo suala la wahadhiri peke yao, siyo suala la wanafunzi peke yao ni suala la wanachuo, mawazo yenu lazima yafanyiwe utafiti kwa kushirikiana na wahadiri wenu na ni lazima tuwe na machapisho zaidi,” Amesema DKt. Ndumbaro
Lakini pia ameagiza kuongezwa kwa lugha zaidi kwa sababu diplomasia pia ni mawasiliano na unawasiliana na watu wa lugha tofauti tofauti.
Vifo kutokana na Corona vyafika laki nne Duniani
Dkt. Ndumbaro amesikiliza changamoto zinazowakabili wanafunzi chuoni hapo, na ameuagiza uongozi wa chuo kuandaa na kuratibu mafunzo kwa vitendo, kutoa huduma stahiki kwa wanafunzi wenye ulemavu/maitaji maalumu ili waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Jeremia Ponera amemhakikishia Naibu Waziri kuwa chuo kitayafanyia kazi na kuyatekeleza maagizo yote aliyoyatoa.
Lissu rasmi kinyang’anyiro Cha Urais 2020 “sitajificha kijijini kipindi cha majanga”
TANESCO Mtwara yazidiwa na kasi ya wananchi kuunganisha umeme