Makamu mwenyekiti wa CHADEMA na aliyekuwa mbunge wa singida Mashariki Tundu Lissu ametangaza nia ya kugombea Urais katika Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Amesema hayo leo Juni 8,2020 akiwa nchini ubeligiji ambapo amesema endapo atachaguliwa kuwa rais ataunda sera thabiti za kiuchumi na kuhakikisha kuwa inabaki kuwa uangalizi wa biashara na kusimamia maslai ya wananchi ikiwemo kuthibiti bei za bidhaa kwa ukuaji wa wananchi.

“Endapo nitachaguliwa, nitarudisha mamlaka ya Bunge kama zamani, nitaondoa vifungo na mateka yaliyowekwa kwenye mahakama zetu na nitaheshimu uhuru wa Mahakama katika wajibu wao wa kutenda haki”amesema Tundu Lissu

Amesema pia endapo atachaguliwa atahakikisha amawafariji wananchi pale wanapokuwa na majanga Kama ya asili na magonjwa ya mlipuko na hata enda kujificha kijijini kwao

Idara ya Polisi ya mji alipouawa Floyd yavunjwa

Aidha amelezea uhalali wake wa kugonmbea nafasi hiyo, ”mimi nina sifa zote za kuwania nafasi yoyote katika nchi hii na wala sijapoteza sifa hizo kutokana na Spika Job Ndugai kunifutia ubunge. Sijawahi kutuhumiwa wala kuthibitika kuwa na makosa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ”amesema Lissu

Na kuongeza “Ninaelewa masuala ya Kimataifa kwa mapana sana. Katika mabara yote, Bara la Australia tu ndio sijatembelea, Nina uwezo wa kuwafuta machozi.”

Tundu lisu anakuwa ni kada wa tatu kutangaza nia ya kugombea Urais kupitia tiketi ya CHADEMA huku wengine wakiwa Ni Dk Meyrose Majige, Peter Msigwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa ambaye pia ni mbunge wa Iringa mjini

Serikali kutoweka bei elekezi zao la Pamba

Zaha afunguka baada ya miaka mitano
Mkwasa: Wachezaji hawana utimamu wa mwili