Hatimaye mshambuliaji Wilfried Zaha amefunguka kuhusu wakati mgumu zaidi aliowahi kukabiliana nao wakati yupo Manchester United ni uvumi kwamba alikua na mahusiano na binti wa aliyekuwa kocha klabuni hapo, David Moyes.

Zaha ambaye kwa sasa anaitumikia Crystal Palace, alikuwa na kipindi kigumu Old Trafford kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, huku muda mwingi alijikuta akitolewa tu kwa mkopo.

Baada ya kucheza mchezo wake ya kwanza Man United chini ya Moyes, Zaha alishindwa kupata nafasi zaidi na baada ya hapo alicheza michezo mitatu tu zaidi. Uvumi ulizagaa zaidi mitaani ukidai kwamba kitendo cha Zaha kulala na binti wa Moyes, mrembo Lauren, ndiyo sababu ya kushindwa kupangwa.

Zaha mwenyewe amesema kwamba jambo hilo lilimpa wakati mgumu sana kwa sababu kutoka kwenye klabu hakuna hata mtu mmoja aliyempa ushauri namna ya kukabiliana na tatizo hilo na zaidi ya hapo, aliachwa tu mwenyewe apambane na hali yake.

Wilfried Zaha opens up about Moyes' daughter rumours
Binti wa Moyes, mrembo Lauren.

“Hakuna yeyote kutoka kwenye klabu aliyeniambia kitu, sikuwa na ufahamu kabisa nini nifanye,” amesema Zaha.

“Nakumbuka niliposti kitu kwenye Twitter nikiandika ‘uvumi wa kipuuzi’ kwa sababu mambo yalikuwa yamezidi sana na baada ya hapo, klabu ilinitumikia meseji ‘hukupaswa kufanya hivyo, usingefanya hivyo’ na hilo niliona kama hawajanisaidia kitu.

“Nikawa mimi mwenyewe napambana, huku watu wakiniambia kwamba sipangwi kwa sababu nimelala na binti yake kocha.”

Zaha alitolewa kwa mkopo kwenda Cardiff City, baada ya kuwa chini ya Moyes kwa miezi mitano tu, na aliporejea kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, kocha huyo Mskochi tayari alikuwa ameshafukuzwa.

Akatolewa tena kwa mkopo na kurejea Crystal Palace kabla ya klabu hiyo ya London maarufu kama The Eagles kuamua kumchukua jumla jumla.

Serikali yaagiza Chuo cha Diplomasia kuongeza tafiti, machapisho
Lissu rasmi kinyang'anyiro Cha Urais 2020 "sitajificha kijijini kipindi cha majanga"