Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Watu wenye Ulemavu ili kukuza ustawi wa kundi hilo katika kuchochea shughuli za maendeleo.

Ameeleza hayo katika tamasha la kimataifa la familia yenye furaha la Watu wenye Uziwi na usikivu hafifu, lililofanyika jijini Dar es Salaam ambapo tamasha hilo lilihusisha pia mshindano la kumsaka mrembo, mtanashati pamoja na mwanamitindo bora duniani mwenye Uziwi na kwamba Rais, Dkt. Samia anawapenda na kuwajali Watu wenye Ulemavu na ndio maana serika imeunda wizara mahususi ili kuwasimamia.

Amesema, Serikali imefufua vyuo vya Watu wenye Ulemavu kwa kutumia Tsh. Bilioni 3.4 kukarabati miundmbinu ambayo imechakaa katika vyuo 6 na kwamba kwa mwaka wa fedha 2023-2024 Serikali imetenga Bil. 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vipya vitatu vya ufundi stadi ili kuongeza udahili wa vijana wenye Ulemavu kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Kuhusu kuimarisha utambuzi wa mapema wa watoto wenye Ulemavu, amesema Serikali imeandaa mwongozo wa utambuzi wa mapema na afua staki kwa watoto wenye Ulemavu na kwamba itaendelea kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kiuchumi kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Tamasha hilo limehusisha washiri zaidi ya 200 kutoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.

LATRA yatangaza ongezeko jipya la Nauli
Kisa Nigeria: Niger yaanza kutumia Umeme wa jua