Serikali nchini Uturuki, imewataka watawala wa Serikali ya Taliban nchini Afghanistan kutengua uamuzi wao wa kuwazuia wanawake kujiunga na vyuo vikuu, ikisema kitendo hicho sio cha kiislamu wala ubinadamu.
Akizungumza na vyombo vya Habari, Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema kitendo hicho si sawa na kuhoji aina ya madhara ya kibinadamu yanayoweza tokea ikiwa wanawake kupata elimu.
Hata hivyo, marufuku hiyo ya utawala wa Taliban ambao uliahidi kulegeza sheria watakapoingia madarakani baada ya kumalizika vita vya miongo miwili, imekosolewa na viongozi mbalimbali duniani.
Aidha, tayari Serikali zingine za nchi ya Marekani na Uingereza zimetoa msimamo wao na kulaani uamuzi huo wa Taliban kuwazuia wanawake kupata elimu ya vyuo vikuu na kusema huo ni uvunjifu wa haki za kibinadamu.