Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unatoa taswira kuwa Watanzania wanaweza kujitengenezea mambo makubwa wao wenyewe bila kupata msaada kutoka sehemu nyingine.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Desemba 22, 2022 mara baada ya kushuhudia tukio la ujazaji maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuongeza kuwa licha ya uwepo wa changamoto kadhaa lakini hii leo nchi inaingia katika historia ambayo ilitarajiwa na kusubiriwa kwa muda mrefu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kufunga geti li maji yaweze kujaa katika Bwawa la Mwalimu Nyerere hii leo Desemba 22, 2022.

Amesema, “Ndugu zangu siku ya leo ni ya kihistoria na hii inaonesha kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitengenezea mambo makubwa yenyewe, na kutokana na ukubwa wa Bwawa hili unaofikia kilometa 100, ni wazi kuwa zitapatikana fursa mbalimbali na kuinua uchumi wa nchi.”

Aidha, amesema maji yanayopita katika Bwawa hilo ni mengi na kwamba ni matumaini yake yatasaidia jamii kupata maji safi na salama hali ambayo itapunguza adha ya wananchi kuwa na shida ya maji katika maeneo mbalimbali hasa yanayozunguka eneo hilo ikiwemo na jiji la Dar es Salaam.

Agram Grant atua rasmi Chipolopolo
Serikali yabanwa zuio la wanawake kujiunga vyuo vikuu