Serikali nchini Kenya imeyapiga marufuku makanisa matano likiwemo lile la mshukiwa wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie aliyewataka waumini wake kufunga hadi kufa.
Kupitia tangazo lililowekwa kwenye Gazeti la Serikali na Msajili wa mashirika nchini humo imeeleza kuwa, leseni ya mhubiri huyo Mackenzie wa kanisa la Good News International Ministries, imefutwa kuanzia Mei 19, 2023.
Licha ya sababu ya kutokula ikionekana kuwa ni chanzo kikuu cha sehemu kubwa ya watu zaidi ya 400 kufariki, ripoti za kitabibu za upasuaji zinaonesha wengine wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa au kubanwa pumzi hadi kufa.
Aidha, marufuku hiyo pia imeyakumba makanisa mengine manne likiwemo la New Life Prayer Centre and Church la mhubiri Ezekiel Odero ambaye anahusishwa kushirikiana na Mackenzie.
na anachunguzwa kwa mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji, itikadi kali na utakatishaji fedha.