Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa Shilingi Trilioni 11.4 za serikali baada ya kushinda kesi za nje na ndani ya nchi zilizokuwa zikiikabili Serikali ikiwemo kesi ya ndege iliyokamatwa Afrika kusini na Canada ambazo walipambana kuhakikisha wanashinda.
Hayo yamebainishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gabriel Malata Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali katika utendaji kazi wao iliyofanyika jijini Dodoma.
Aidha ofisi hiyo imefanikiwa kuokoa mashamba 106,hotel viwanja ambavyo vimerejeshwa katika Shirika la Reli na nyumba ambazo nazo zimerejeshwa kwa wahusika.
Wakili Mkuu Malata amesema kutokana na kazi hizo muhimu ambazo wanafanya mawakaili ndio maana wameandaa semina hiyo ya siku tatu ambayo wanaamini itawajengea uwezo.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na sheria Amon Mpanju aliwapongeza ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutokana na kuandaa Semina hiyo ambayo wanaamini italeta manufaa makubwa kwa Mawakili kutokana na kwamba watapata muda wa Kujifunza.