Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kundi la ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mpina amesema kuwa Wilaya zilizopo mipakani mwa nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo, hivyo amemuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada ng’ombe hizo.
“Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” amesema Mpina.
Aidha, amesema kuwa ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika na kuitaka kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na kuhakikisha mifugo yote inapatikana.
-
Naibu Waziri wa Nishati atembelea kituo cha kusambaza Umeme
-
Tanesco waweka kambi Mbezi
-
Rais Magufuli atumiwa ujumbe na Jakaya Kikwete
Hata hivyo, kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahawa Mrindoko amesema kuwa ng’ombe hao waliokamatwa ni mali ya raia wa Rwanda, ambapo amesema kuwa sheria itachukua mkondo wake.