Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati katika jiji la Dodoma ukiwemo wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato na Barabara za mzunguko, kuzingatia ubora na viwango na ukamilishaji wa kazi kwa wakati.

Senyamule ameyasema hayo hii leo Februari 15, 2023 wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo, wa Uwanja wa Ndege, barabara ya mzunguko LOT 1 inayotoka Nala-Veyula-Mtumba-Ihumwa yenye urefu wa kilometa 52.3 na LOT 2 yenye urefu wa Kilometa 60 inayotoka Dry pot Ihumwa, Ngo’ngo’na, Matumbulu, Bihawana – Nala.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akipokea maelekezo ya ukamilishaji wa miradi hiyo..

Amesema, “Mradi huu ni wa aina yake barani Afrika na tunataka ukamilike ndani ya muda, sote tunafahamu umuhimu wa kukamilika 2024 au mapema 2025, dhamira ya serikali ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuhikisha utekelezaji wa miradi hii unazingatia utoaji wa huduma kwa jamii (CSR), kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na miongozo iliyopo.”

Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato Lot 1 sehemu ya kwanza utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 165 na Lot 1 sehemu ya 2 utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 199, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa amemtama Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo la abira, ili liweze kukamilika kwa wakati na kwenda sambamba na ujenzi wa njia za kuruka na kutua ndege.

Familia ya marehemu 'AKA' yatoa taarifa hii mpya
Tanzania, Angola wasaini makubaliano tume ya kudumu