Serikali imetangaza awamu ya pili ya ajira kwa Walimu 5000 ili kufikia idadi ya Walimu 13,000 kutokana na kibali kilichotolewa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Akihutubia Mkutano wa Pili wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Joseph Nyamhanga amesema, awamu ya Pili ya ajira hizo itafanyika mapema mwaka huu.
Awamu hiyo ya Pili inafanyika baada ya walimu waliopata ajira za awamu ya Kwanza 8,000 kuripoti kazini.
Walimu hao 5,000 watapelekwa Vijijini na kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa.