Serikali Nchini, imeongeza zaidi ya Shilingi 11 Bilioni kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 kutoka Bilioni 1.097 hadi kufikia Bilioni 12 kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja.
Meneja wa Wakala ya Barabara ya Vijijini na Mijini – TARURA Wilaya ya Kilosa, Mhandisi Harold Sawaki ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Ruhembe lenye urefu wa mita 40 itakayogharimu Shilingi Bilioni 1.28.
Amesema, Fedha hizo, ni sehemu ya kuhudumia mtandao wa Barabara zenye urefu wa Km 913.67 zinazosimamiwa na Wakala ya Barabara ya Vijijini na Mijini – TARURA, Wilayani Kilosa ambapo pia alifungua barabara inayounganisha Kata ya Ruhembe na Mikumi – Ifakara (2km), itakayogharimu Shilingi 203 Milioni 203.
Miradi hiyo, itakapokamilika itaondoa kero za Wananchi ambazo walikuwa wakizipata hapo awali ikiwemo kuwafikisha barabara kuu na kwamba ujenzi wa daraja la Berega lenye urefu wa mita 140 linalogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7.9 upo katika hatua za mwisho za umaliziaji.