Takriban Watu 10 wameuawa wakiwemo watoto, na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya kutekelezwa shambulio la bomu kwenye kanisa moja mjini Kasindi katika mpaka wa DRC na Uganda.
Tukio hilo, limeripotiwa kutokea kilometa 80 kaskazini mwa mji wa Beni ambapo Waasi wa ADF wenye uhusiani na mtandao wa Al Qaeda wametajwa kuhusika.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi eneo la Kasindi, Luteni Mopero Momitabonge amesema, “Watu wameumia wengi, wengine wako hosipitalini zaidi ya kumi na wawili na bado tunafuatilia tuki hili.”
Shambulio hilo linatokea licha ya uwepo wa operesheni za pamoja za kijeshi zinazoendelea kwenye eneo hilo dhidi ya waasi hao, kati ya jeshi la Serikali (FARDC), kwa ushirikiano na lile la Uganda, UPDF.