Jumla ya watu watatu wameuawa katika shambulizi la bunduki kwenye hoteli inayopendwa na wafanyabiashara wa kichina katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Shambulizi hilo la Desemba 12, 2022 limeoshuhudiwa kwa milipuko kadhaa pamoja na milio ya risasi uliopelekea moshi kufuka kutoka kwenye jengo la ghorofa la hiyo ya Kabul Longan Hotel na maafisa wa ualama wa Taliban walionekana wakikimbia kulizingira eneo lilipo jengo hilo.

Hali ilivyokuwa baada ya shambulizi kwenye eneo la Kabul Longan Hotel. Picha ya Arab News Pakistan.

Aidha, wanausalama wa Taliban wanasema wameimarisha usalama tangu walipoingia madarakani Agosti mwaka jana, licha ya mji wa Kabul kukumbwa na miripuko kadhaa ambayo kundi linalojiita Dola la Kiislamu linakiri kuisababisha.

Msemaji wa polisi mjini Kabul amesema waliouawa ni washambuliaji watatu, na kuongeza kuwa wageni wote wa hotel wameokolewa na hakuna raia wa nchi za nje aliyepoteza maisha na tayari Helikopta inapiga doria juu ya hoteli iliyoshambuliwa.

Rafiki wa Waziri Mkuu auawa kwa risasi
Waziri Mkuu kuanza ziara Mkoa wa Rukwa